Duration 1:4

Makafani ya hospitali ya rufaa ya Nyamira yafungwa Kwa mda ili kufanyiwa ukarabati

1 122 watched
0
5
Published 30 May 2023

Makafani ya hospitali ya rufaa ya Nyamira imefungwa Kwa mda ili kufanyiwa ukarabati kutokana na hali mbaya ya chumba hicho cha kuhifadhia maiti. Ukarabati huu unafuatia lalama kutoka kwa wenyeji kuhusu hali mbaya ya makafani hiyo. Akizungumza katika makao makuu ya kaunti hiyo mjini Nyamira, waziri wa afya Dkt. Ombati Mokua amesema miili yote kutoka makafani hiyo na ile itakayotoka katika hospitali ya rufaa ya Nyamira, itahifadhiwa kwenye makafani ya hospitali jirani ya Kinara hadi ukarabati utakapokamilika. Barabara ya kuelekea makafani hiyo vilevile itakarabatiwa.

Category

Show more

Comments - 0