Duration 8:2

NENO LA KALVARI : AMBWENE MWASONGWE

266 822 watched
0
3.2 K
Published 28 Dec 2020

Mungu amekuwa mwema sana kwangu, pamoja na kupitia changamoto nyingi mwaka 2020, zikiwemo za kuuguliwa, kufiwa, bado nilipoteza watu muhimu sana, marafiki na washirika wenzangu wa huduma. Katikati ya huzuni, hofu, misiba, magonjwa Mungu alinipa wimbo huu, ambao umekuwa na maneno ya maombi na ukiri wangu mbele zake, na hakika Bwana amenisaidia sana. Nakuombea kwa Mungu unapousikiliza ukaponye moyo wako, utakapokumbuka uliyopitia, iwe kupoteza ndugu, marafiki, kazi, uchumi, ndoa, mahusiano, biashara, iwe umepitia vifungo na kukamatwa Bado Mungu ndiye Baba kwako na amekusaidia sana. Yawezekana hali ingekuwa mbaya zaidi ya hapo, hayo uliyoyaona ni ishara kwamba Mungu amekusaidia. Nakushauri sikiliza kwa kurudia mpaka wimbo ukae ndani yako na Mungu aliyenivusha mimi atakuvusha nawe pia. Kama unamjua mtu yeyote aliyepitia kipindi kigumu mwaka 2020 basi mwalike ausikilize wimbo huu. Barikiwa sana

Category

Show more

Comments - 749