Duration 1:36

Aliempiga kibao Ali Hassan Mwinyi afariki dunia.

19 734 watched
0
60
Published 2 Aug 2020

SHUJAA IBRA! Jumanne ya March 10 mwaka 2009 kijana Ibrahim Saidi (pichani) maarufu kama "Sultani" alimzaba kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, wakati wa baraza la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee, tukio lililoibua taharuki kubwa ukumbini hapo na nchi nzima kwa ujumla. Baada ya tukio hilo Mzee Mwinyi alisema amemsamehe kijana huyo, lakini Polisi walimkamata na kumfungulia mashtaka ya shambulio la kudhuru mwili. March 11 alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, ambapo alikiri kosa na kufanya shauri hilo kusikilizwa kwa siku moja tu kabla ya kutolewa hukumu. Ibra alisema sababu ya kumtandika kibao Mzee Mwinyi ni kutokana na kuzungumzia masuala ya kondomu kwenye baraza la Maulidi ambapo ni kinyume na mafundisho ya dini yake. March 13 mwaka 2009 Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Neema Chusi, alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela. Kabla ya kusomewa hukumu hiyo Ibra alipewa nafasi ya kuiomba mahakama impunguzie adhabu lakini alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kumpunguzia adhabu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee. _ “Mimi ni kiumbe dhaifu, hakimu ni kiumbe dhaifu, na sote ni viumbe dhaifu mbele ya Mwenyezi Mungu. Siwezi kuiomba mahakama inipunguzie adhabu, ila namuomba Mwenyezi Mungu anipunguzie adhabu ya kaburi. Na kama akitaka nipunguziwe adhabu mnayotaka kunipa hakuna wa kuzuia” alisema Ibra. Baada ya kutumikia adhabu yake kwa miezi 8 alipata msamaha wa Rais na kuachiwa huru, lakini June 02 mwaka 2019 alifariki dunia nyumbani kwake Mabibo Loyola jijini Dar.!

Category

Show more

Comments - 14