Duration 6:24

Fanya mambo haya 3, kila siku asubuhi.

4 154 watched
0
49
Published 8 Mar 2022

Ni kwanini ukiamka asubuhi unajikuta hauna shahuku ya kufanya chochote, au hauna amani katika moyo wako? Hali hii ni ngumu kuikwepa ukiwa kama binadamu, inaweza kuwa imeisha kukuta au bado ijakukuta lakini inaweza kuja kukukuta. Lakini napenda kukumbusha usi vushe vushe video hii ili uweze kusikila kwa makini na kujua mambo haya muhimu. Lakini kama ni mgeni usisahau ku subscribe. Kila asubuhi tukiamka kuna mambo ambayo tunashindwa kujua umuhimu wake, na leo ntakuletea mambo matatu tu ambayo unatakiwa kufanya kila uwamkapo, mambo haya yatasaidia akili, mwili hata kiafya, Kumbuka mwili wa binadamu ukiwa usingizini huwa unahusisha viungo vingi kurelux(kutofanya kazi), tukiachana hivyo viungo vya mwili kutofanya kazi au kutoshughurika mfano mikono, miguu na videlo pia mwili unakuwa unashindwa kuhusisha misuli ya sehemu hizo kushughurika. Sasa ni jambo gani ambalo nataka ulifanye kila ukiamkapo. Je ushawai kuona hizi dalili pale uwamkapo 1. Kichwa kuuma 2. Mwili kukosa nguvu 3. Macho kuuma 4. Msongo wa mawazo Dalili hizi huwa zinatukumba sana, pia watu wengine hujisikia vibaya na kwenda kumuona daktari, lakini tambuwa kuwa, hali hii inaweza mkuta kila mwanadamu katika siku zote za maisha yetu, na leo nimekuletea mambo muhimu matatu,(3) ambayo yatakusaidia kuwa sawa kila uwamkapo kama ukiyafata, Endapo ukiamka adubuhi zingatia kufanya mambo muhimu yafuatayo, 1. Kunywa maji, Miili yetu inaundwa na asilimia 82% ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo. Kwa wale wasio weza kunywa maji ausubuhi, basi wanashauliwa kunywa maji ya vugu vugu maana, asilimia kubwa ya watu huwa wanashindwa kunywa maji ya kawaida wakihisi wanatapika au watatapika. Zifuatazo ni faida zakunywa maji Asubi, A. Huondoa sumu mwilini Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu. B. Huboresha metaboli Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema. Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa ajili ya watoto na watu wazima pia 2. Fanya mazoezi, Kuna aina ya mazoezi ambayo yanafaa kufanya Asuhi, sio lazima ukimbie au kunyanyua vyuma, ila kuna mazoezi ya kunyoosha misuli ambayo yatakusaidia . Pia si lazima ufanye mazoezi yote unayo yajua kwa wakati mmoja kama yanakushinda, chagua ambayo unayoweza anza nayo kila zoezi jaribu kulifanya ndani ya dakika 2 na nusu.Ukifanikiwa kufanya mazoezi haya utauweka mwili na akili yako katika hali nzuri na kukusaidia kufanya kazi zako kwa ufanisi zaidi. Faida ya mazoezi ya asuhi ni muhimu katika mifumo ya homoni Mfano homoni ya testosterone ambazo husaidia kukupa nguvu na hamu ya kufanya kazi huwa katika damu kwa kiasi kikubwa wakati wa asubuhi – hivyo, kukupa nguvu, uwezo na hamu ya kufanya mazoezi. Pia testosterone husaidia kujenga misuli na kuchoma mafuta, mojawapo ya nia ya kufanya mazoezi. Mazoezi pia husaidia kuongeza kiwango cha kemikali au vichocheo viitwavyo endorphins – maarufu vichochea furaha. Endorphins hutufanya kujisikia raha na kuwa wenye furaha. Ukifanya mazoezi wakati wa asubuhi kiwango cha endorphins kitaongezeka katika damu na mwili wako, hivyo kukufanya mwenye furaha siku nzima – kitu ambacho kitakusaidia kufanya shughuli zako vizuri 3. Kuoga, Nimeweka mbinu ya kuoga kuwa ya mwisho, kwasababu kabla ujaoga inatakiwa ufate utaratibu huu na mtililiko huu nilio kuonesha, watu wengi wakiamka huwa wanakimbilia bafuni kuliko kuuweka mwili sawa yaani kiakili na kiafya, hivyo sababu ya kuoga inataka ufate mbinu mbili nilizo taja apo juu, sasa tuangalie faida ya kuoga asubuhi. husaidia kuboresha hali yako, hupunguza mafadhaiko na wasiwasi, na kupunguza uchovu Fanya hivi kila siku ili uwe imala siku zote, pia usisahau ku subscribe. #on_trending #music #millardayo

Category

Show more

Comments - 12